Jumatatu, Juni 02, 2014

FIFA 2014 BRAZIL..10 DAYS LEFT: AJABU YA KWANZA KUTOKA FIFA 2014 BRAZIL...HAIJAWAHI KUTOKEA KABLA

Siku kumi kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza, tutaanza kuhesabu siku zilizosalia kwa kutazama mawili matatu kuhusu michuano hiyo.
Je unafahamu kuwa BRAZIL 2014:
Hii itakuwa mara ya kwanza teknolojia ya golini kutumika katika Kombe la Dunia. Kutakuwa na kamera 14 katika kila paa ya kila uwanja utakaotumika. Kamera 7 zitakuwa zinatazama goli moja, na 7 nyingine goli jingine. Kamera hizo zimeunganishwa kwenye kompyuta ambayo itatathmini kila mpira utakapopigwa. Mpira unapovuka tu mstari wa goli refa atahisi mtikisiko katika saa maalum atakayokuwa amevaa mkononi. Pia atapata ujumbe mfupi wa maandishi kupitia saa hiyo unaosema "Goli".

0 comments:

Chapisha Maoni