Jumatatu, Juni 02, 2014

CHADEMA WATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO

Kufutia kifo cha mjumbe wa kamati kuu ya chadema Shida Salum ambaye ni mama yake Mzazi na Zitto zuberi kabwe chama cha demokrasia na maendeleo kimetangaza siku tatu za maombolezo.
Akiongea na wananchi waliokuwa wamejitokeza kwa wingi mtaa wa balaa ukiwa ni mkutano wa madiwani na mbunge wa Arusha mwenyekiti wa chadema wilaya ya Arusha Mhe. Nanyaro Ephata alisema si busara kuendelea na mkutano huo huku wakiwa wamempoteza kiongozi wa ngazi za juu kabisa za maamzi.

0 comments:

Chapisha Maoni