Jumamosi, Juni 14, 2014

MWANAMKE AVAMIWA NA MAPANGA NA WATU WASIOJULIKANA

Katika tukio jingine, Jumanne Joel (30), ameuawa na wananchi baada ya kumvamia Monica Lutonja (32) wa Kijiji cha Nyankumbu, Kata ya Kalangalala mjini Geita, na kumjeruhi kwa mapanga.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi ambapo inadaiwa Joel akiwa na wenzake watatu, walifika kwa mama huyo wakidai kuwa marafiki wa kaka yake, na alipofungua walianza kumshambulia kwa mapanga hadi akapoteza fahamu.
Kamanda Konyo alisema watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa, ili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

0 comments:

Chapisha Maoni