Sakata la kusambaa picha zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za
watu maarufu hapa nchini leo limezungumziwa tena katika bunge la
Tanzania kule Dodoma ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Mhe.
Habib Mnyaa ameonekana akihoji serikali inachukua hatua gani juu ya watu
wanaotuma picha zao zisizo na maadili mitandani zikiwemo za kina Wema
na Diamond wanazopiga wakiwa chumbani na kuweka kwenye mitandao.
Katika majibu yake waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof.
Makame Mbarawa anasema
Mhe. Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni zitakazokuwa zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti.
0 comments:
Chapisha Maoni