Maabara ya shule ya sekondari ya arusha iliyowai kutoa viongozi wengi wa serikali na kituo cha sayansi kwa shule za sekondari za mkoa wa arusha ipo
katika hali mbaya ya uchakavu unaosababisha maji ya mvua kuingia ndani
hali inayodaiwa kuchangia kupunguza ari ya wanafunzi kujiunga na
masomo ya sayansi.
Wakizungunza na wanahabari wanafunzi wa shule ya sekondari ya arusha
wamesema uchakavu wa maabara hiyo umechangia kufifisha juhudi za
wanafunzi wa masomo ya sayansi kwani wakati wa masika walazimika kukosa
mafunzo ya vitendo kwakuwa wananyeshewa na mvua wanapokuwa ndani ya
maabara hiyo hivyo wameiomba serikali iwasaidie.
Kwaupande wake mmoja wa wajumbe wa bodi ya shule hiyo michael
sanga amekiri hali hiyo kuwa kikwazo katika kuongeza ubora wa elimu na
kuongeza kuwa serikali imetoa kiasi cha shilingi milioni hasini za
kufanya ukarabati wa baabara hiyo na sasa anatafitwa mkandarasi na mkuu
wa shule hiyo christopher malamsha amesema ukarabati huo utapokamilika
ari ya wanafunzi katika masomo ya sayansi itaongezeka.
0 comments:
Chapisha Maoni