Jumapili, Juni 08, 2014

KUHUSU SAKATA LA DEREVA NA TINGO KUCHOMA MOTO LORI LA DHANDO, MSIKILIZE HAPA KAMANDA MUNGI AKIELEZEA TUKIO

Siri imefichuka sababu ya malori ya mizigo na mafuta kuungua moto baada ya jeshi la polisi mkoani hapa kuwashikilia watu sita akiwemo dereva na utingo wa lori aina ya Scania, mali ya Kampuni ya Dandu wakidaiwa kuchoma moto lori hilo.
Ilidaiwa kwamba jamaa hao wakazi wa Mbeya walifanya hivyo baada ya kutaifisha mzigo wa mitumba na viatu wenye thamani ya shilingi milioni 100 waliokuwa wakiusafirisha kwenye lori hilo kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ilidaiwa kuwa wawili hao walifanya njama ya kulichoma moto lori hilo baada ya kushusha mzigo huo na kuuhifadhi kwenye Kijiji cha Maguhani Mufindi ili kuuza kutokana na dereva wa lori hilo kudaiwa kodi ya shilingi laki 4 na baba mwenye nyumba.
Sasa msikilize kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi akisimulia tukio hilo>>>>>>>

0 comments:

Chapisha Maoni