Jumapili, Juni 08, 2014

MFAHAMU MCHEZA FILAMU WA SIKU NYINGI TZ, MAREHEMU MZEE SMALL

Mzee Small alizaliwa mwaka 1955 na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, pia Mzee Small kila ulipozungumza naye alikuwa na kawaida ya kujitamba kuwa yeye ndiye alikuwa msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha katika luninga.
Pamoja na kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa kuonyesha vichekesho kupitia luninga, lakini bado amesimama kufanya maigizo ingawaje alianza sanaa hiyo miaka 30 iliyopita na alipata kufundishwa na Bw. Said Seif ‘Unono’ (ambaye kwa sasa ni marehemu).
Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, pia Mzee Small amecheza sanaa katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.

0 comments:

Chapisha Maoni