Jumapili, Juni 08, 2014

JINSI HARUSI YA MBUNGE JOSHUA NASSARI NA MKEWE ANANDE NKO ILIVYOFANA JANA ARUSHA

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Samwel Nassari jana amefunga ndoa na Anande Nko kwenye Kanisa la Pentekoste lililopo Kilinga, Arumeru jijini Arusha ikifuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika Viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hoteli ya Ngurdoto.
Sherehe hiyo ilianza saa 7:00 mchana ambapo watu wote walialikwa wakiwemo ndugu, marafiki, jamaa na wananchi wote wa Arumeru Mashariki ambao wamepiga 'mpunga' wa kutosha na vinywaji hadi kila mtu akaondoka akisema 'Nassari ameacha historia'.

0 comments:

Chapisha Maoni