Jumatano, Juni 11, 2014

KELLY ROWLAND AJITANGAZA KUWA MJAMZITO

Mwimbaji wa Marekani Kelly Rowland ameonekana kuthibitisha taarifa kuwa ni mja mzito.
Huu utakuwa uja uzito wa kwanza kwa msanii huyu wa zamani wa kundi la Destiny's child.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kelly amebandika picha ya jozi mbili za viatu, vikubwa na vidogo huku akisema 
Nitakuwa wa kuvutia kama baba yangu....
Kelly na Tim Witherspoon walioana mwezi Mei mwaka huu nchini Costa Rica, na miongoni mwa wageni waalikuwa walikuwa Beyonge na mdogo wake Solange.

0 comments:

Chapisha Maoni