Mshambulizi wa Arsenali Olivier Giroud alifunga bao
na kuiongoza ''Le Blues'' kuilaza Jamaica mabao 8-0 katika mechi yao
ya mwisho ya kujipima nguvu iliyochezwa siku ya Jumapili.
Ufaransa ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0 kufikia
muda wa mapumziko, Yohan Cabaye, Blaise Matuidi na Karim Benzema
wakimpa kocha Didier Deschamps kila sababu ya kutabasamu kabla ya
kudundadunda .
Matuidi na Benzema walifunga tena
katika kipindi cha pili, huku bao lake Giroud na mengine mawili kutoka
kwa Griezmann yakitamatisha ushindi wao.
Ufaransa itakabiliana na Honduras, Uswizi na Equador katika kundi E.
Kiungo cha kati wa Real Madrid Benzemaalionyesha
mchezo wa kuridhisha huku Ufaransa ikionyesha kwamba inaweza kujikimu
bila Franck Ribery ambaye hatahudhuria michezo ya Kombe la Dunia kutoana
na jeraha la mgongo.
Hugo Lloris anaychezea Tottenham Hotspurs,
Patrice Evra wa Manchester United, Mamadou Sakho wa Liverpool na Moussa
Sissoko wa Newcastle walicheza mechi hiyo.
Hapo baadae, beki wa Asenali na Loic Remy wa Queens Park Rangers waliingia kama wachezaji wa ziada.
0 comments:
Chapisha Maoni