Jumamosi, Mei 17, 2014

MPENZI WA SAMIR NASRI AWAUDHI WAFARANSA BAADA NASRI KUACHWA NA TIMU YA TAIFA KATIKA FIFA 2014 BRAZIL

Chama cha soka cha Ufaransa kimepokea kwa hasira ujumbe ulioandikwa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na rafiki wa kike(Mpenzi) wa Samir Nasri.
Mapema wiki hii kiungo huyo wa Manchester City hakujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kitakachoenda Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia licha ya kuonyesha uwezo mkubwa na kuisaidia klabu yake kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza.

Mpenzi wake alitwaye,Anara Atanes alitumia mtandao wa Twitter kuonyesha hasira zake,ambapo aliandika,**** Ufaransa.Pia alimshambulia kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ufaransa,Didier Deschamps.
Atanes aliandika: 
F*** Ufaransa na f*** Deschamps! Nani s*** meneja!
Binti huyo alionyesha kukazia pointi yake,huku akirudi mtandaoni tena na kusema: 
Kama huku soma tweet yangu vizuri..nitarudia binafsi…f*** Ufaransa na f*** Deschamps!
Mwanamitindo huyo alitumia tena Twitter siku ya Alhamisi usiku kuomba radhi kwa chochote alichokosea,ila alikataa kuomba radhi kwa Deschamps.
Huku akisisitiza:”Naomba msamaha kama nilimkosea mtu yeyote kutoka Ufaransa,ujumbe wangu kupitia Tweeter haukuwa lengo kwa nchi nzima kwa ujumla.”
Hivyo ikimaanisha kuwa ujumbe wa binti huyo ulimlenga moja kwa moja meneja wa timu ya Taifa ya Ufaransa pamoja na jopo lake la benchi la ufundi na sio kwa wananchi wa Ufaransa.
Didier Deschamps aliyewahi kuzinoa klabu za Monaco,Marseille na Juventus alishindwa kumjumuisha Samir Nasri kikosini kwa madai ya kwamba nyota huyo hana mchango kwenye timu ya Taifa ukilinganisha na klabuni kwake Manchester City.
Kitendo hicho kilizua maswali kwa watu wengi hususa kwa mashabiki wa klabu yake ambao walishuhudia kiungo huyo mshambuliaji akiisaidia vilivyo timu yao mpaka kufanikiwa kushinda makombe mawili msimu huu.
Nasri alipoulizwa alipokeaje taarifa za kutochaguliwa alisema,
Nilijiandaa kabisa.Nilifahamu kabla,mara nyingine unakuwa na hisia.
Huku akielezea kuwa,
Unapokuwa unataka kuzungumza na meneja,lakini yeye hataki kuzungumza na wewe,unafahamu kuwa hauendi kwenye kombe la dunia.

0 comments:

Chapisha Maoni