MTANGAZAJI aliyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya
runinga Bongo, Maimartha Jesse, amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa
za kuongeza makalio.Habari za moto kutoka kwa sosi wa kuaminika,
zinasema kuwa Maimartha ambaye pia huitwa Mai amefikia hatua hiyo baada
ya yeye kutumia na kufanikiwa.
Hamshangai siku hizi kila staa anaonekana kuwa na makalio makubwa? Ni kazi ya Mai hiyo. Anafanya hiyo biashara muda mrefu sana. Ni za kunywa na kupaka.
Mbona hata yeye ametumia dawa hizo muda mrefu sana? Ukimwangalia utagundua zamani hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni kwa sababu ya dawa
alisema sosi huyo. Akaongeza:
Hata Lulu Semagongo (Aunt Lulu) ndiye aliyemsababishia kuwa na makalio makubwa kwani wakati wako karibu alikuwa akimpa dawa hizo.
Waandishi wetu walifika dukani kwa Mai bila kujua kama ni waandishi
na kuulizia bidhaa hizo ambapo zilitolewa, wakapiga picha bila
kugundulika.
Mai akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa mapaparazi waliokuwa na njaa
ya habari, aliwaambia:
Ni dawa nzuri, mara moja zinarekebisha umbo na unakuwa wa kuvutia. Kuna za shilingi 250,000 na 260,000 inategemea kama ni vidonge au losheni.
Mapaparazi wetu walipompigia simu Mai baada ya kutoka dukani hapo na
kumweleza kuhusu uuzaji wa dawa hizo dukani kwake, alisema duka lake
linauza urembo wa aina zote kwa mastaa na wasio mastaa.
Kama nimetumia dawa za kuongeza makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi duka langu linadili na urembo wa aina zote
alisema Mai akishindwa
kufafanua zaidi.
Lulu alipovutiwa waya na kuulizwa kama makalio yake ni matokeo mazuri
ya dawa za Mai alisema: Sijawahi kutumia dawa za Mai kwa ajili ya
kuongeza makalio.
Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa nawaelekeza kwa Mai.





0 comments:
Chapisha Maoni