Alhamisi, Mei 08, 2014

KATONI ZA VIROBA DOUBLE PUNCH NA CHARGER ZAKAMATWA NA POLISI MBEYA

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lakamata pombe kali [viroba] aina ya Double Punch katoni 04 na Charger katoni 06. Bidhaa hizo zilikamatwa baada ya kufanyika msako katika eneo la njia panda kasumulu, kata ya Ngana, tarafa ya Unyakyusa, wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya jana majira ya saa 15:30 alasiri. Mtuhumiwa alikimbia na kutupa mzigo baada ya kuwaona askari. Juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Askari wa jeshi nchini Tanzania akiwa amelala baada ya kulewa kiroba! Sio mtuhumiwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed  Msangi anatoa wito kwa jamii kutoa taarifa za watu wanaowatilia mashaka katika maeneo yao ili uchunguzi zaidi ufanywe dhidi yao. Aidha anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya kwani ni hatari kwa afya zao na ni kinyume cha sheria. Halikadhalika kwa wafanyabiashara kuacha kujihusisha na uuzaji wa pombe kali zilizopigwa marufuku na serikali kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

0 comments:

Chapisha Maoni