Rais wa Nigeria , Goodluck Jonathan,amewaambia
washiriki wa mkutano wa kiuchumi unaofanyika mjini Abuja kuwa utekaji
nyara wa zaidi ya wasichana 200 na kundi la wapiganaji wa kiislamu wa
Boko Haram inaashiria mwanzo mpya katika vita dhidi ya ugaidi nchini
Nigeria .
Hayo yamewadia huku maafisa wa utawala wake
wakijitetea vikali dhidi ya shutma za kushindwa kukabiliana na wimbi la
mashambulizi kutoka kwa kundi hilo.
Msemaji wa serikali Doyin Okupe,
amekanusha kuwa jeshi la taifa hilo limezidiwa nguvu na waasi hao au
utawala wa taifa umeshindwa.
Aidha msemaji huyo anasema kuwa jeshi lina kazi
ya kujaribu kuwalinda raia na kupunguza maafa kwani litakaposhambulia
waasi lazima maisha ya wananchi yalindwe.
Maelfu ya watu wanaaminika kuuawa katika msururu
ya mashambulio katika siku za hivi karibuni katika mji wa Gamboru
Ngala, walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji wenye silaha walishambulia
umati katika masoko na nyumba za watu.
Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekahu alikiri
kuwateka nyara wasichana hao wengi wao walio kati ya umri wa miaka 16
na 18 na kusema kuwa atawauza kwani hawakupaswa kuwa shuleni toka mwanzo
na kwamba badala yake wanapaswa kuolewa.
Wasichana wengine 11 walitekwa nyara Jumapili baada ya vijiji viwili kushambuliwa karibu na maficho ya wapiganaji hao.
Utekaji nyara wa wasichana hao umesababisha
serikali ya Nigeria kulaumiwa na kukosolewa kwa kujikokota katika hatua
zake dhidi ya wapiganaji hao.




0 comments:
Chapisha Maoni