Ni miaka nane ilikuwa imepita bila kuwasikia kundi la Wagosi Wa Kaya
kutoka Tanga, lakini ‘ghafla bin vuu’ weekend iliyopita jina lao
limeanza kurudi tena katika vichwa vya habari baada ya kutambulisha
nyimbo zao mbili mpya.
Dr.John na Mkoloni wa kundi la Wagosi wa Kaya wamesema wanafahamu kuwa wana deni kubwa kwa mashabiki wao, hivyo wameanza kulililipa kwa kuachia nyimbo mbili mpya kwa mpigo ambazo ni ‘Bao’ na ya pili inaitwa ‘Gahawa’ zote zikiwa na video.
Dr.John na Mkoloni wa kundi la Wagosi wa Kaya wamesema wanafahamu kuwa wana deni kubwa kwa mashabiki wao, hivyo wameanza kulililipa kwa kuachia nyimbo mbili mpya kwa mpigo ambazo ni ‘Bao’ na ya pili inaitwa ‘Gahawa’ zote zikiwa na video.
Kuthibitisha kuwa ujio wao sio wa kubahatisha Wagosi wamesema kuwa
wamejiandaa vizuri kukabiliana na soko gumu la muziki hata upande wa
album ambao unakimbiwa na wasanii wengi kwa sasa.
“katika hilo hilo soko ambalo limevurugika tunao uwezo Wagosi wa Kaya
kwa watu kupenda album yetu na wakainunua”, alisema Dr. John “kutokana
na nguvu ya mashairi yetu na inategemea muziki tunaokuja nao muziki
gani.”
Akizungumza kupitia kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM Dr. John aliendelea,
“Kwa muziki wa kipindi kile msanii jambo la kwanza kabisa
analolitegemea yeye ni kwenye mauzo ya album, unapata hela nyingi sana
kwa kupitia album, milioni 20, 25, 15, 18 inategemea na nguvu yako kwa
kipindi kile lakini. Lakini kwa kipindi hiki kidogo wadau wenyewe
wanaouza album wanalalamika kwamba siku hizi teknolojia imekuwa kubwa
sana wezi wengi mauzo kidogo yameshuka lakini hawaachi wanaendelea bado
kama kawaida, ni kweli lakini pia kwasababu ambazo wanazitoa siku hizi
ni show sana na mambo mengine madogo madogo ambayo yanalipa.”
Wagosi wamesema album yao mpya itakayoitwa ‘Uamsho’ itazungumzia mambo mbalimbali.
“Mfano watu wanajua kwamba Wagosi Wa Kaya wakija wao ni siasa kwenda
mbele tu hapana, sisi tuneshaimba vitu vingi sana, tumeshaimba Wauguzi,
tumeshaimba Trafiki, Soka la bongo, Ubia, Kilimo, tumeshaingia kila
kona, zile nyimbo zipo tu, na huu ni uamsho na album yenyewe inakuja
inaitwa Uamsho, tunaamsha”.
Nyimbo zote mbili ‘Gahawa’ na ‘Bao’ zimerekodiwa katika studio ya
Tongwe Records huku video zake zimeshootiwa Tanga na kampuni ya Ngome
Videos chini ya muongozaji Mecky Kaloka.
0 comments:
Chapisha Maoni