Jumapili, Aprili 13, 2014

HII NI KUFURU, WALIOALIKWA KWENYE HARUSI YA MTOTO WA RAIS WA NIGERIA GOODLUCK JONATHAN WAZAWADIWA iPHONE GOLD

Sijui unaweza ukaitafsiri vipi hii lakini katika tafsiri ya kawaida utabaini kuwa viongozi wa afrika hawataki kutoka kwenye uongozi ukweli ni kwamba kuna mkwanja mrefu huko cheki hii.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan ametoa zawadi ya shukrani ya simu aina ya iPhone kwa kila mgeni mwalikwa aliyeudhulia sherehe ya ndoa ya mwanae wa kike wa kwanza,Faith iliyofanyika Abuja Ecumenical Centre.
Ukiachana na mzee Goodluck kutapika simu hizo zenye gharama kwa wageni, pia ndoa hiyo ilikuwa ikirushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha NTA.
Kama ambavyo zilikuwa zimeandikwa kwenye bos simu hizi wengine ilikuwa ni ndoto kwao kumiliki simu hii lakini bahati imekuwa kwao wamejipatia zawadi hii mhimu simu ambayo kila mtu anatamani kuimiliki.

0 comments:

Chapisha Maoni