Jumapili, Aprili 13, 2014

YONDANI ALIPA FADHILA KWA BABA YAKE

Beki wa Yanga, Kelvin Yondani, amemhamisha mji baba yake mzazi mzee Patrick Yondani kutoka Mwanza na kuhamia Dar es Salaam.
Yondani amekuwa na mafanikio makubwa katika kuichezea Yanga kutokana na umahiri wake ambapo amekuwa akiisaidia kutokana na kuwa beki bora.
Chanzo cha kuaminika kutoka Mwanza kinachokaa karibu na mzee huyo, kimeeleza kuwa, beki huyo wa Yanga ameamua kumhamisha mkoa baba yake mzazi kwa kumjengea nyumba ya kifahari maeneo ya Kigamboni ili aishi naye.
“Unajua baba Yondani haishi Mwanza kwa sasa, kwani mwanaye Kelvin amemhamisha, anaishi Dar baada ya kumjengea nyumba.
“Kwa sasa makazi yake makubwa yapo Kigamboni, ndipo alipojengewa nyumba ya kisasa kabisa,” kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa baba Yondani kulizungumzia suala hilo, alisema: “Ahaaa, haa, unajua mimi nimekuja Dar kumtembelea kijana wangu tu mara moja na muda si mrefu nitarejea Mwanza ila sijajua nitarudi lini.
“Hayo ni mambo ya watu tu bwana, kotekote ni nyumbani, nitarudu tu Mwanza.”
Jitihada za kumpata Yondani ziligonga mwamba, kwani siku yake ya mkononi ilikuwa ikiita tu kwa muda mrefu bila kupokelewa.

0 comments:

Chapisha Maoni