MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’
amesema anashindwa kumtathimini msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby
Madaha kutokana na kujitenga na wasanii wenzake.
“Hana kadi ya chama chochote na isitoshe anajitenga na wasanii
wenzie, hahudhurii kwenye shughuli yoyote ile iwe ya huzuni au furaha,
kiukweli simuelewi, abadilike,” alisema Steve.
Paparazi wetu alipomtafuta Baby Madaha kuzungumzia ishu hiyo alisema
ana mambo mengi ya kufanya ndiyo maana huwa hashirikiani na wenzake,
akipata nafasi atahudhuria.
0 comments:
Chapisha Maoni