Wapiga kura nchini Iraq watashiriki katika zoezi la
upigaji kura katika mikoa yote isipokuwa mkoa mmoja katika uchaguzi wa
kwanza wa wabunge tangu wanajeshi wa Marekani waondoke nchini humo mwaka
2011.
Waziri mkuu wa sasa Nouri al-Maliki atagombea
kiti chake kwa muhula wa tatu lakini kampeni zimekuwa zikipigwa kwa
misingi ya vurugu za kisiasa zinazoendelea kukithiri nchini humo.
Selikali ya muungano ya bwana Maliki
inayoongozwa na chama cha Kishia imekabiliwa na wakati mgumu kupambana
na uasi unaongozwa na kundi lenye ufungamano na Al Qaeda katika mji wa
Falluja na mkoa wa Anbar.
Sauti za mizinga zimekua taswira ya kila siku katika baadhi ya maeneo ya Iraq wakati kampeni za kuelekea uchaguzi huu.
Matokeo yake ni mashambulio ya kujitolea mhanga karibu kila siku.
Uchaguzi kufanyika Iraq |
Helikopta za kijeshi zinashika doria katika anga
ya Baghdad na serikali imefunga uwanja wa ndege na baadhi ya barabara
kuu ndani na nje ya mji huo.
Hatua hizo zinanuia kuwapa imani wapigaji kura watakaojitokeza kwani ni bayana kuwa huenda vituo vya kupigia kura vikalengwa.
Watu 160 wameuawa wiki iliyopita huku wengine 275 wakijeruhiwa.
Baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa vikosi vya
usalama vimepoteza maafisa elfu moja mwaka huu kwenye mapigano ya
kukabiliana na uasi katika maeneo ya Fallujah na Anbar.
Inatabiriwa kuwa huenda Bw Maliki akashinda
awamu ya tatu na kumuwezesha kuunda serikali ya muungano lakini ni
bayana kuwa swala la usalama litasalia kuwa changamoto kubwa.
0 comments:
Chapisha Maoni