Wanasayansi nchini Marekani wanasema watu waliowahi
kupata maradhi ya moyo wanaweza kuishi maisha marefu iwapo watakula
zaidi vyakula ambavyo havijapitia viwandani.
Watafiti walichunguza zaidi ya watu elfu nne
waliowahi kupata mshituko wa moyo na kubaini kuwa wana uwezekano mkubwa
wa kuishi miaka tisa zaidi kama watakula vyakula hivyo .
Vyakula ambayo havijapitia viwandani vina
nyuzinyuzi ambazo tayari imethibitishwa kuwa husaidia katika kuwezesha
binadamu kwenda haja bila matatizo.
Vyakula ambayo vina nyuzinyuzi hizo ni kama vile matunda, mboga na nafaka.
Hatahivyo wataalam wanasema watu katika mataifa mengi hawali vyakula hivyo kwa wingi.
0 comments:
Chapisha Maoni