
Mourinho ameshindwa kuficha hisia zake za kumtamani
nyota huyo ambaye kwasasa yuko benchi akiuguzi goti lake na kuna ripoti
kuwa anafikiria kuondoka Ufaransa baada ya kucheza kwa mwaka mmoja
kutokana na Ligi Kuu ya nchi hiyo kukosa ushindani.
Akihojiwa Mourinho
pia aliondoa uwezekano wa kuhitaji
huduma ya washambuliaji wa timu ya Paris Saint-Germain Zlatan
Ibrahimovic na Edinson Cavani.
Mourinho amesema ana timu lakini hana
mshambuliaji na Falcao ni kama hana timu kwasababu mchezaji wa kiwango
kama chake hastahili kucheza mbeke ya mashabiki 3,000.
Mourinho alienda
mbali na kudai kuwa Monaco ni klabu ambayo mchezaji anaweza kumalizia
soka lake wakati akiwa ameanza kuchuja.
Falcao mwenye umri wa miaka 28
alijiunga na Monaco kwa paundi milioni 50 akitokea Atletico Madrid
katika majira ya kiangazi mwaka jana.
0 comments:
Chapisha Maoni