Jumanne, Aprili 29, 2014

BATULI LAWAMANI KUVURUGA NDOA YA MTUNIS

HABARI za motomoto kutoka vyanzo vya uhakika, zinasema kuwa staa wa kike anayekuja juu kwa sasa katika tasnia ya filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ameitikisa ndoa ya mwigizaji mwenzake, Nice Mohammed ‘Mtunis’ kwa madai ya kutoka naye kimapenzi.
Chanzo chetu, kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini kilifunguka kuwa ishu ya wawili hao kuwa wapenzi siyo siri, kwani mara kadhaa wamekuwa wakijiachia sehemu mbalimbali, huku mke wa Mtunis akinyetishiwa, jambo lililosababisha migongano ndani ya ndoa hiyo.
Mmechelewa kweli kujua! Leo ndiyo mnauliza kuhusu Mtunis na Batuli? Hao ni wapenzi na penzi lao limenoga kwelikweli sasa hivi. Imefikia hatua Mtunis na mkewe hawana maelewano mazuri. Nyumba ni kama inayumbishwa na Batuli lakini Mtunis hataki kumwacha Batuli
kilipasha chanzo hicho.
 Kama ada, Risasi Mchanganyiko lina desturi ya kupata mzani wa habari kabla ya kuirusha, ndivyo ilivyofanyika kwa Mtunis ambaye aliposomewa mashitaka yake alipovutiwa waya, alikanusha vikali akidai ndoa yake ina amani na hana uhusiano na Batuli.

Kwanza nani amekuambia kuwa mimi natoka na Batuli? Yule ana mtu wake na mimi nina ndoa yangu. Sikia kaka, katika kipindi ambacho ndoa yangu ina amani ni hiki, sitaki kabisa haya mambo. Mtakuja kusababisha Batuli agombane na mumewe kisa mimi
alisema Mtunis kwa sauti ya juu.
Batuli alipopatikana kwa njia ya simu, alikuwa msikivu muda wote alipoelezwa kuhusu madai hayo, mwishoni akajibu kwa mtindo wa kuuliza: 
Kwanza nikuulize, Mtunis ni Muislam au Mkristo?
Mwandishi wetu alipomjibu kuwa ni Muislam, akaendelea: 
Sasa kipi cha ajabu hapo? Kwa imani yake ya Kiislam, ana ruhusa ya kuoa wake hadi wanne. Halafu kuna wakati nilishaishi naye miaka si chini ya minne, kwa hiyo sioni ajabu hapo. Hata kama ikitokea tena hakuna tatizo.
Achana na watu bwana, acha tu watu waongee. Lakini ninachosema hakuna cha ajabu hapo. Maisha yanaruhusu, yaani kisheria hata Mungu anaruhusu - siyo ajabu. Siwezi kuzungumza zaidi maana nimesafiri nipo kwenye harusi, dada yangu anaolewa.

0 comments:

Chapisha Maoni