JIJI la Dar es Salaam na vitongaji vyake, limekumbwa na maafa ya vifo vya watu,uharibifu wa miundombinu huku mamia ya watu wakikosa makazi, kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana.
Mvua hizo zilisababisha tatizo kubwa la usafiri kutokana na barabara kujaa maji, kuezua nyumba na kuua watu na kuacha maelfu ya wakazi wa jiji hilo bila makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa.
Mvua hiyo ilianza kunyesha majuzi usiku ikiambatana na radi na ngurumo nzito na kusababisha kukatika mara kwa mara kwa umeme katika baadhi ya maeneo ya jiji hilo ambalo ni kitovu kikuu cha biashara na uchumi kiujumla.
Madaraja ya Bagamoyo yalivunjika na kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria wanaotumia madaraja hayo.
Madaraja mengine yaliyovunjika ni pamoja na daraja la Msewe na la mto wa Ng’ombe, huku magari yaliyokuwa yakienda Mwananyamala, Mikocheni yakitokea Ubungo yakilazimika kusitisha safari zake baada ya kujaa maji.
Baadhi ya maeneo ya jiji hasa Kigogo, Tandale, Mabibo na Tabata yalikumbwa na kadhia ya maji kujaa kwenye makazi yao na kusababisha usumbufu ambao ulionekana kutishia usalama wa mali na maisha.
Wazee walikuwa wakihangaika huku na kule kutafuta sehemu za kujisitiri, lakini vijana na watoto walionekana wakicheza kwenye mvua bila kujali mustakabali wao.
Wafanyabiashara wa vyakula vya jumla na rejareja katika baadhi ya maeneo waliamka na kukuta sehemu kubwa ya bidhaa zao zimeharibika huku meza na vyombo vya mama lishe, vikionekana kuelea barabarani baada ya kusombwa na maji.
Mmoja wa wamiliki wa zahanati moja iliyoko Kigogo Darajani ambaye jina lake halikufahamika mara moja, alisema amepata hasara baada ya maji kuingia ndani na kuharibu vifaa mbalimbali vya hospitali zikiwamo dawa.
“Angalia, nimepata hasara sana. Mpaka sasa wasaidizi wangu wanafanya kazi ya kuzoa maji na kusafisha vitanda na baadhi ya vifaa, vingine havifai,” alisema mmiliki huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina.

0 comments:
Chapisha Maoni