Jumapili, Aprili 13, 2014

MAKAMU WA RAIS GHARIB BILAL, SULEIMAN KOVA, SAID MECKY SADICK WANUSURIKA KIFO KWENYE AJALI YA NDEGE

MAKAMU wa Rais Dk. Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na mpiga picha wa TBC, George Kasembe wamenusurika kifo baada ya helkopta waliyokuwa wanasafiria kupata ajali Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Viongozi hao walikuwa katika helkopta ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa ziara ya kukagua athari za mafuriko jijini Dar es Salaam.
Baada ya ajali, viongozi hao wamepatiwa matibabu katika majeraha waliyoyapata na wameendelea na ziara yao!

0 comments:

Chapisha Maoni