Jumapili, Aprili 13, 2014

ARUSHA YAPIGWA BOMU

Mlipuko mkubwa umetokea leo majira ya saa 1.30 usiku katika baa maarufu ya Arusha night park "Matak0 bar" iliyopo eneo la Mianzini mjini Arusha.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa mlipuko huo unatokana na bomu lililotengwa katika eneo la bar hiyo na kujeruhi watu zaidi ya 20 waliokuwa wakiangalia mchezo wampira wa miguu ligi kuu ya England kati ya Chelsea na Swansea.

Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya dk. Mohamed na Mount Meru. Mashuhuda wanaeleza kuwa kuna baadhi ya majeruhi wamekatika viungo kama miguu nakadhalika.

Hili ni tukio la tatu mjini arusha bomu kurushwa na kutegwa katika maeneo ya mikusanyiko ya watu na hadi sasa Polisi hawajawahi kukamata wahusika wa matukio yote matatu.

0 comments:

Chapisha Maoni