Mtu aliyefahamika kwa jina la Mashaka Mwashimbili anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kukutwa na bangi kiasi cha gramu 905, siku ya jumamosi saa 4:45 usiku huko Tunduma.
Taarifa kutoka kwa maafisa wa polisi zinasema kuwa Mashaka Mwashimbili 23, Mnyiha , mkulima na mkazi wa Mogombani mjini Tunduma alikutwa akiwa ameficha bhangi nyumbani kwake katika mfuko wa plastiki na kukamatwa na askari waliokuwa katika msako.
Mtuhumiwa tayari yupo mahabusu na taratibu nyingine zinafuatwa ili afikishwe mahakamani.
Aidha kamanda wa polisi na kamishshna msaidizi wa jeshi la polisi Diwani Athumani ametoa wito kwa jamii kuacha mara moja tabia ya kutumia dawa za kulevya kwani ni hatari kwa afya ya mtumiaji na ni kinyume cha sheria.
0 comments:
Chapisha Maoni