Jumatano, Agosti 21, 2013

KIJANA WA MIAKA 17 AKUTWA AMEKUFA KICHAKANI MBEYA


Mwanafunzi wa kidato cha tatu 17, amekutwa vichakani akiwa ameuawa na watu wasiojulikana huko katika kitongoji cha Itange, kijiji cha Madabaga, wilaya Mbalali mkoani Mbeya tarehe 19/08/2013 majara ya 12:00 asubuhi.

Taarifa toka kwa maafisa wa polisi zinaeleza kuwa Hans Hamis Mbogo, Msangu na mkazi wa Madabaga ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Katenga ameuawa na watu ambao bado hawajafahamika mpaka sasa na kasha kutelekezwa vichakani.
Aidha taarifa hiyo inasema kuwa Hans alikuwa wendesha pikipiki (boda boda) na alikuwa na pikipiki yake yenye namba za usajili T.263 BZC aina ya T-BETTER ambayo ilikodishwa na nwatu wasiofahamika kwa lengo la kuwapeleka kijiji cha jirani waliomuua na kutoweka na pikipiki hiyo.
Mwili wa marehemu ambao umekutwa na matundu saba mgongoni yaliyotokeza mbele ya golori za bunduki aina ya gobole umekutwa vichakani jana majira ya saa 12:oo jioni umekwisha fanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu tayari kwa mazishi.
Pamoja na hayo kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Diwani Athumani ametoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa juu ya waliohusika na tukio hiloazitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

0 comments:

Chapisha Maoni