Jumapili, Agosti 18, 2013

GONGO BADO TATIZO MBEYA


Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa na pombe ya moshi (GONGO) juzi majira ya saa 10:15 jioni katika eneo la MAKUNGURU, jijini MBEYA.
Taarifa toka jeshi la polisi zimewataja watuhumiwa hao kuwa ni ANATARIA MATUMA, 24, mnyakyusa na mkulima, NOAH MWANGOKA,31, myakyusa na mkulima pamoja na MASUMBUKO JAILOS,28, msafwa na mkulima wote wakiwa ni wakazi wa MAFIATI jijini hapa.
Pamoja na hayo, taarifa zinasema kuwa watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na pombe hiyo haramu kiasi cha lita 3 na kutajwa kuwa ni watumiaji wa kilevi hicho na tayari watuhumiwa wote wako mahabusu na taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.


Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa jeshi la polisi, Diwani Athumani ametoa wito kwa jamii kuacha matumizi ya pombe haramu kwani ni kinyume cha sheria na pia ni hatari kwa afya.

0 comments:

Chapisha Maoni