Alhamisi, Septemba 14, 2017

UNAFAHAMU KUHUSU UVUMBUZI WA LIFTI?

Taswira ya lifti za kisasa

Imekuwa kawaida kwa dunia ya sasa haswa katika majengo marefu na yenye ghorofa nyingi kutumia lifti ili kutoa msaada wa kufika katika vyumba vya juu kwa urahisi, unajua mwanzo wa ubunifu wa lifti zenyewe na mtu aliyeumiza kichwa?
Uvumbuzi wa lifti ulifanyika kiasi cha miaka 237 iliyopita.
Mvumbuzi wa lifti hiyo ya kwanza alikuwa ni raia wa Marekani na tunamfahamu kwa jina la John Bikbart. 
Lifti hiyo ilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza katika mji wa Chicago nchini Marekani. 
Moja ya picha za lifti za mwanzo
Katika majaribio hayo, watu kadhaa waliingia ndani ya lifti hiyo na kwenda juu na chini. 
Lifti ya kwanza ya umeme ilitengenezwa mwaka 1889, huku ile ya otomatiki ikitengenezwa mnamo mwaka 1915.

0 comments:

Chapisha Maoni