UTAFITI uliofanywa na Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kati ya mwaka 2006 na 2015 unaonesha kwamba wanaume wanakufa kwa wingi zaidi kuliko wanawake.
Aidha vifo hivyo vilikuwa vikitokea zaidi katika umri wa miaka kati ya 35 na 39. Akitoa taarifa ya utafiti kwa wadau wa Afya mkoani Dodoma, hivi karibuni, Mtafiti Mkuu Mwandamizi, Dk Leonard Mboera alisema pia katika kipindi hicho, kati ya vifo 247, 976 vilivyotokea, moja ya tano ya vifo hivyo viliwakumba watoto wa chini ya miaka mitano.
Dk Mboera alisema katika utafiti huo uliofanyika katika hospitali 39, vifo vingi vya wanaume vilitokea katika hospitali za mikao ya Mara, Kilimanjaro, Kigoma, Pwani, Ruvuma, Rukwa, Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza.
“Ukichukua vifo hivyo na kuangalia wastani utabaini kwamba vifo vingi vinatokea wa watu wa umri wa miaka 31 ambapo katika umri huo wa miaka hiyo, wanaume waliofariki ni 33 na wanawake ni 29,” alisema.
Alisema zaidi ya asilimia 57.6 ya vifo vilivyotokea, vilitokana na magonjwa ya kuambukiza, uzazi na magonjwa yanayotokana na lishe duni, wakati asilimia ya vifo 35.7 vilitokana na magonjwa yasiyoambukiza wakati asilimia 6.7 vifo vilitokana na ajali na maumivu nje ya mwili.
0 comments:
Chapisha Maoni