Kiwanda cha mimea cha idara ya utafiti wa mimea ya taasisi ya sayansi ya
China chenye ukubwa wa hekta 20 kilizinduliwa mwezi Juni mwaka jana
mjini Quanzhou, mkoani Fujian, China.
Katika banda la kilimo lisilo na vumbi na vijidudu, mboga mbalimbali zinakua kwenye rafu bila udongo na mwanga wa jua. Wafanyakazi wanadhibiti joto, unyevu, mwanga wa taa za LED, hewa ya Carbon Dioxide na mbolea kupitia kompyuta. Tatizo la ukuaji wa mimea kutegemea majira na hali ya hewa limetatuliwa, na mboga zinaweza kuzalishwa kiwandani kwa mfululizo mwaka mzima.
Wafanyakazi wanapoingia kwenye banda la kilimo, wanatakiwa kujisafisha mara nyingi, kuvaa nguo mbili za kikazi, barakoa na glavu, ili kuzuia vijidudu na wadudu kuingia ndani ya banda hilo. Hivyo mboga hizi hazijawahi kumwagiliwa dawa za kuwaua wadudu hata kidogo.
Mkurugenzi wa kiwanda hiki Bw. Pei Kequan alisema mboga hizi hazina hata haja ya kusafishwa kabla ya kupikwa, kwani mazingira ya kiwandani ni safi zaidi kuliko maji ya bomba.
Hivi sasa kiwanda hiki kinaweza kuzalisha tani 1.5 za mboga zisizo na uchafuzi kwa siku, na mboga hizi zimeuzwa katika miji mbalimbali mkoani Fujian.

0 comments:
Chapisha Maoni