Kila ifikapo majira ya joto, msitu wa Saihanba
unakuwa na mandhari ya kupendeza. Upepo unavuma kwenye misonobari, mimea
mingi inakua kando ya mito, wadudu na ndege wanatoa milio, mambo yote
hayo yamewavutia watalii wengi.
"Mazingira ya hapa ni mazuri, anga ni ya rangi ya buluu na inapendeza sana."
"Hali ya hewa ya hapa ni safi na mandhari ni nzuri. Mji wa Beijing kuna
msongamano mkubwa wa watu na magari. Nimekuja ili kujipumzisha."
Taasisi ya misitu ya China imekadiriwa kuwa, msitu wa Saihanba si kama
tu unasaidia kuhifadhi rasilimali ya maji na kusafisha maji, bali pia
inaweza kutoa hewa ya Oxygen inayokidhi mahitaji ya watu milioni 2
katika mwaka mmoja.
Wakati watalii wanapohisi upepo wa fufutende
unaopita msitu wa misonobari, ni vigumu kwao kujua jinsi msitu huo
ulivyopandwa katika miaka mingi iliyopita. Mfanyakazi mstaafu wa shamba
la msitu huo Bw. Zhang Baozhu anasema
"Zamani upepo wenye mchanga
ulivuma hapa mara kwa mara. Katika majira ya mpukutiko, upepo
ukipeperusha mchanga ulikuwa wa manjano, na katika majira ya mchipuko,
upepo ukipeperusha theluji ulikuwa mweupe. Wakati upepo ulipopeperusha
mchanga mwingi, ilitubidi kuwasha taa nyumbani ili tuweze kuona vizuri."
Mwaka 1962, serikali ya China ilianzisha shamba la msitu wa Saihanba.
Wafanyakazi 369 ambao wastani wa umri wao ni chini ya miaka 24
walikwenda kwenye shamba hilo lenye mazingira magumu ambayo theluji
inakuwepo kwa miezi 7 kila mwaka, na joto linaweza kufikia nyuzi 43
chini ya sifuri katika majira ya baridi. Jambo linalowasikitisha zaidi
ni kwamba katika miaka miwili ya mwanzo, chini ya asilimia 8 ya miti
walioyopanda ilistawi. Mkuu taasisi ya shamba la msitu wa Saihanba Bw.
Cheng Shun anasema,
"Mwanzoni tuliagiza miti midogo kutoka nje,
lakini hatukuweza kutatua suala la kukuza miti midogo. Kupanda miti
inahusu mambo mengi, ikiwemo kuchimba miti midogo kutoka sehemu
nyingine, kuisafirisha kwa treni, na kuipeleka milimani. Kosa lolote
litasababisha miti hiyo kufa."
Kaskazini mwa msitu wa Saihanba
wenye urefu wa mita 1500 kutoka usawa wa bahari, ni jangwa la
Hunshandake ambalo ni moja kati ya majangwa kumi makubwa nchini China,
na kusini nwa msitu huo ni miji ya Beijing na Tianjin. Zamani upepo
wenye mchanga uliingia Beijing kupitia eneo hilo, lakini sasa msitu huo
umezuia vizuri mchanga wa jangwani kupeperushwa kusini. Takwimu
zinaonesha kuwa siku zenye mchanga na vumbi angani katika majira ya
mchipuko mjini Beijing zimepungua kwa asilimia 70 kuliko miaka 50 karne
iliyopita. Hali ya hewa na mazingira ya msitu wa Saihanba pia
imeboreshwa, sasa aina 1,757 za wanyama na mimea inaishi katika msitu
huo.
Wafanyakazi wa shamba la msitu wa Saihanba wanaanza
kufikiria matumizi endelevu ya rasilimali za msitu huo. Naibu mkuu wa
shamba hili Bw. Chen Zhiqing anasema,
"Kanuni yetu ni kutoa
kipaumbele uendelezaji wa msitu na mazingira ya kiviumbe. Rasilimali za
msitu zinatakiwa kutumiwa kwa mujibu wa sayansi badala ya kufuatilia
faida tu. Tunashikilia maendeleo endelevu ya msitu huo kwenye msingi wa
kuhifadhi mazingira ya kiviumbe."
Kuanza mwaka 2012, shamba la
msitu wa Saihanba lilianza kupunguza ukataji wa miti kwa kiasi kikubwa.
Mapato kutoa mauzo ya mbao yalipungua na kufikia chini ya asilimia 50
kutoka asilimia 90 ya mapato yote. Wafanyakazi wamejitahidi kuendeleza
shughuli za kukuza miti midogo, utalii na uzalishaji wa umeme kwa nguvu
ya upepo, na pia wamejionea mabadiliko kwenye maisha yao. Wafanyakazi
wengi wamepata nyumba mpya katika kaunti ya Weichang iliyoko karibu
zaidi na msitu huo, na wengi wamenunua magari. Mfanyakazi Yang Liying
anasema,
"Napapenda sana hapa, zamani nilifikiri maisha ya hapa
ni magumu, lakini nilitakiwa kuishi hapa kwa sababu wazazi wangu
walitaka kuishi hapa. Lakini siku hizi mazingira ya hapa ni mazuri sana,
mshahara pia ni mkubwa."
Takwimu zinaonesha kuwa msitu wa
Saihanba unaweza kuleta mapato ya yuan milioni 600 kila mwaka kwa maeneo
yaliyoko kando ya msitu huo.
Hellow Nice Blog! Visit https://www.bongoexclusive.net
JibuFuta