Jumanne, Agosti 08, 2017

KUNG'ARISHA MENO NI HATARI KWA UIMARA WA MENO YAKO

Watu wengi wanatamani kuwa na meno meupe yenye kung'ara sana kwaajili ya kuboresha urembo au utanashati wao, hapa hutumika njia nyingi kuyasafisha hayo meno hata kwa njia zisizo salama.
Ni kweli tabasamu linanoga zaidi pale unapokuwa na meno safi, na wengi huamini meno ya njano huwa ni machafu hata kama yameswakiwa, na wengi wao huyachukia meno ya aina hiyo.
Ziko sababu nyingi hupelekea mtu kuwa na meno ya njano, mfano wenzangu wa Kilimanjaro wao meno yao huwa njano kutokana na aina ya maji watumiayo, lakini pia uvutaji sigara, ugoro, aina fulani za pombe na hata kutoyasafisha mara kwa mara.
Sasa wataalamu wanasemaje? Kitaalamu unaambiwa rangi halisi ya meno ni njano na si nyeupe angavu, pia tunaapiwa wale wenye kuyatakatisha meno yao na kuondoa rangi halisi pia huondoa uimara wa meno yenyewe. Muhimu ni kuendelea kuyasafisha kwa mswaki na dawa zinazoshauriwa na wataalamu wa kinywa pasipo kulazimisha kubadili rangi na kuwa angavu ili uendelee kulinda meno yako.
Leo umefahamu kuhusu hili kupitia Fichuo, karibu wakati mwingine ufahamu mengine zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni