Jumanne, Mei 16, 2017

MMOJA WA MANUSURA WA LUCKY VINCENT APASULIWA BEGA NA TAYA, KESHO KUPASULIWA TENA

Mmoja kati ya manusura watatu wa ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent amefanyiwa upasuaji wa bega ‘shoulder’.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imeeleza kuwa mtoto Doreen amefanyiwa pia upasuaji wa nyonga ‘hip’ ambapo baadae leo mtoto huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa taya ‘jaw’. 
Doreen anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine hapo kesho ambapo itakuwa ni katika uti wa mgongo ‘spine’.

0 comments:

Chapisha Maoni