Jumatatu, Mei 15, 2017

LITA 4694 ZA KUTENGENEZEA DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA DAR ES SALAAM

Kamishna wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga amesema wamekamata kiasi cha lita 4,694 za kemikali bashirifu zinazoweza kutengeneza dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mapema leo baada ya kufanya oparesheni maalum iliyofanyika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, Sianga amesema kemikali hiyo imekamatwa katika Mtaa wa Kipepeo eneo la Mwenge jijini hapa.
Aidha amesema pia wamebaini kuwepo kwa maghala mengine yaliyopo Bagamoyo mkoani Pwani na Moshi mkoani Kilimanjaro.

0 comments:

Chapisha Maoni