Watu 26 wamefariki dunia na wengine zaidi ya elfu 28 wamepoteza makazi yao baada ya kaunti 13 za Kenya kukumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.
Chama cha msalaba mwekundu cha Kenya kimesema mafuriko yamesababisha uharibifu mkubwa wa nyumba na miundo mbinu, na pia kukwamisha shughuli muhimu kama vile kilimo na elimu kwenye maeneo mbalimbali nchini Kenya.
Katibu Mkuu wa chama cha msalaba mwekundu cha Kenya Bw Abbas Gullet amesema kwenye baadhi ya maeneo wafugaji wamepata hasara kubwa ya mifugo, amesema kuendelea kwa hasara hiyo, kunaleta taabu zaidi kwa jamii za wafugaji zilizothiriwa na ukame.
Mamlaka ya hali ya hewa ya Kenya imesema mvua kubwa zitaendelea kunyesha katika maeneo kadhaa ya Kenya, hasa maeneo ya magharibi na pwani.
0 comments:
Chapisha Maoni