Waandamanaji huko Paraguay , wamevamia majengo ya bunge la nchi hiyo na kuliwasha moto.
Wanapinga hatua ya bunge la senate la nchi hiyo kukutana kwa faragha na kupitisha mswada wa kufanyia marekebisho kipengee cha katiba ya nchi hiyo,kitakachomruhusu Rais Horacio Cartes kuwania muhula wa pili madarakani.
Watu kadhaa wamejeruhiwa pale Police walipofyatua risasi za mipira na michirizi ya maji ya kasi kujaribu kuwatawanya waandamanaji ili kuzima ghasia hizo.
Waandamanaji hao wanasema mabadiliko hayo yanaharibu misingi na taasisi za kidemocrasia nchini Paraguay .
Hata hivyo Mswada huo huenda ukafanikiwa, kwani sasa unapelekwa katika bunge la daraja la pili ambako Rais Cartes ana idadi kubwa ya wabunge kutoka chama chake.
Mwaka 1992, sheria ilipitishwa kuzuia marais wa Paraguay kuwania muhula wa pili kama suhulu la kukabiliana uditeta na marais kung'angania madaraka..
0 comments:
Chapisha Maoni