Jimbo lililo magharibi mwa India la Gujarat, limepitisha sheria ya kuharamisha kuchinjwa ng'ome na kutangaza adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa yoyote ambaye atapatikana na kosa hilo.
Chini ya sheria hiyo, pia wale ambao watapatikana wakisafirisha nyama ya ng'ome watahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.
Ng'ome hutajwa kuwa mtakatifu na waumini wengi wa Hindu, na kumua ngome ni kitendo haramu katika majimbo mengi nchini India.
Kufuatia sheria hiyo jimbo la Gujarat sasa litakuwa na sheria kali zaidi kuhusu suala hilo nchini India.
Watakaopatikana na hatia watapigwa faini kali na kifungo gerezani. Faini ya kosa hilo imeongezwa kutoka dola 771 hadi dola 1542.
Waziri mmoja katika jimbo la Gujarat, aliawaambia waandishi wa habari kuwa ng'ome ni ishara ya utamaduni wa India
Sheria hizo mpya zitaanza kutekelezwa siku ya Jumamosi.
0 comments:
Chapisha Maoni