Zaidi ya watu milioni 300 sasa wanaishi na huzuni, ambayo ni chanzo kikuu cha afya mbaya na ulemavu duniani kote, kulingana na makadirio ya karibuni kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa lilitoa makadirio hayo siku ya Alhamisi kabla ya Siku ya Afya Duniani.
"Makadirio hayo yanapaswa kutoa wito kwa nchi zote kufikiria upya mtazamo wao katika afya ya akili na kuitibu kwa haraka kama inavyostahili," Mkurugenzi Mkuu wa WHO,Margaret Chan,alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni