Jumanne, Machi 28, 2017

ZUIO LA BIASHARA YA MAZIWA YA MAMA KUTOKA CAMBODIA

Serikali ya Cambodia siku ya Jumanne ilipiga marufuku mauzo ya nje ya maziwa ya mama kutoka kwa wanawake wa Cambodia kwa soko la Marekani na kampuni ya Ambrosia Labs Co. ,kulingana na barua kutoka kwa Baraza la Mawaziri.
"Hatua ya haraka lazima ichukuliwe ili kuzuia mkusanyiko na mauzo ya nje ya maziwa ya mama kutoka Cambodia," Ngor Hongly, waziri wa nchi wa Baraza la Mawaziri, alisema katika barua iliyotumwa kwa Waziri Afya,Mam Bunheng.
Kulingana na makala yaliyochapishwa kwenye Vice.com tarehe 14 mwezi Machi,karibia wanawake 50 ambao wengi wao ni maskini wameajiriwa na kampuni hiyo kuuza maziwa ya mama kwa senti 64 za marekani kwa wakia, na kwa kawaida kila mwanamke kila siku anauza wakia 12 za maziwa kwa siku,na kupata zaidi ya dola 7 za Marekani.
Maziwa hiyo huuzwa katika soko la Marekani kwa hadi dola 4 za Marekani kwa wakia moja.

0 comments:

Chapisha Maoni