Jumanne, Machi 28, 2017

KATIBU MKUU WA CAF AACHIA NGAZI

Ikiwa ni wiki kadhaa tangu Issa Hayatou ashindwe katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa CAF, sasa katibu mkuu wa CAF raia wa Morocco Hicham el Amrani ameamua kubwaga manyanga.
Sababu za El Amrani kujiuzulu hazijawekwa wazi lakini El Amrani amesema ni wakati tu sasa umefika anaona ni bora aachane na uongozi katika chama hicho cha soka barani Afrika.
Katika barua yake El Amrani anasema anajisikia furaha kwamba baada ya miaka 8 ya kazi sasa ameamua kuachana na shirikisho hili la soka (CAF) na kuwashukuru CAF, FIFA na vyama vyote vya soka kwa kumpa nafasi kuleta maendeleo katika soka barani Afrika.

0 comments:

Chapisha Maoni