Jumamosi, Machi 25, 2017

UTEUZI MWINGINE MKUBWA ALIOUFANYA LEO RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hii leo machi 25, 2017 amefanya uteuzi mwingine kwa kumteua Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Taarifa ambazo Fichuo tumezipata kutoka Ikulu ya Dar es Salaam ni kwamba kabla ya Charles Edward Kichere kuteuliwa alikuwa ni Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo ya Mapato nchini.
Baada ya kufanyika kwa uteuzi huo leo, nafasi aliyotoka Charles Edward Kichere itabaki wazi mpaka pale itakapojazwa baadae.

0 comments:

Chapisha Maoni