Jumamosi, Machi 25, 2017

SHAQ O'NEAL AMWAGA MACHOZI SANAMU YAKE IKIZINDULIWA TAPLES CENTER


Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu  wa Los Angeles Lakers ya nchini Marekani Shaquille O'Neal, maarufu kama Shaq mwenye miaka 45 sasa amejikuta akimwaga machozi wakati sanamu yake ilipozinduliwa katika uwanja wa michezo wa Taples Center ishara ya kutambua mchango wake katika mchezo wa kikapu.
Staa huyo aliyewahi pia kuwa mwanamuziki wa Rap (Rapper) na mtangazaji wa sasa katika kiindi cha runinga cha Inside the NBA aliongozana na mchezaji mwenzake Kobe Bryant katika hafla hiyo.
Mwenyewe anasema aiwekeza muda wa kutosha katika mpira wa kikapu na kupata mafanikio makubwa katika maisha yake kupitia mchezo huo japo kuna matukio ya kumuumiza hatoyasahau, lakini hakutegemea kama wapenzi wa mchezo huo wangeutambua mchango wake na hata kumfanya kuwa sehemu ya alama kwao.

0 comments:

Chapisha Maoni