Jumamosi, Machi 25, 2017

BOMBA LA GESI LALIPUKA NA KUATHIRI WATU 28

Watu watatu waliaga dunia na wengine 25 kujeruhiwa wakati bomba la gesi ya kawaida lililipuka siku ya Jumamosi (leo) katika jengo moja la makazi katika mkoa wa Mongolia kaskazini mwa China,serikali za mitaa zilisema.
Ajali hiyo ilitokea karibia saa 2:00 mchana katika jengo lenye ghorofa kadhaa na kusababisha jengo hilo kuporomoka,vyombo vya habari viliripoti. na kuongeza kuwa watu wanne kati ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mahututi.
Operesheni inaendelea ili kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni