Kuwa na watoto inaweza kuchangia mtu kuishi miaka mingi, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa.
Manufaa ya kuwa na watoto huonekana hata wakati watu wanapotimia umri wa miaka 80 na zaidi.
Wataalamu
kutoka kwa taasisi ya Karoliska mjini Stockhom nchini Sweden,
walifuatilia maisha ya mtu kutoka umri wa miaka 60 kwa wanaume wote
(704,481), na wanawakae (725,290) waliozaliwa kati ya mwaka 1911 na 1925
wanaoishi nchini Sweden.
Waligundua kuwa wanaume na wanawake
ambao walikuwa na takriban mtoto mmoja, walikumbwa na vifo vichache
kuliko wanaume na wanawake wasio na watoto.
Katika umri wa miaka 60, tofauti ya miaka ya kuishi
kati ya wale walio na watoto na wasio nao, ni karibu miaka miwili kwa
wanaume na mwaka mmoja unusu kwa wanawake.
Wakifika umri wa miaka
60, wanaume walio na watoto hutarajia kuishi miaka mingine 20.2 huku
wanaume wasio na watoto wakitarajia kuishi miaka 18.4 zaidi ambayo ni
tofauti ya mwaka moja unusu.
Nao
wanawake walio na umri wa miaka 60 walio na watoto hutarajia kuishi
miaka 24.6 zaidi, huku wale wasio na watoto wakitarajia kuishi miaka
23.1 zaidi, ambayo ni tofauti ya mwaka moja unusu.
Utafiti wa awali ulionyesha kuwa watoto wasichana ndio wanaweza kuwasaidia wazazi wao uzeeni kuliko hata watoto wavulana.
Nao uatafiti mpya unaonyesha kuwa wavulana wanaweza kuwasaidia wazazi sawa na wasichana ikiwemo kuwasaidia kupata matibabu.
Hata hivyo watu wasio na watoto hupata wakati mgumu zaidi kupata huduma ambazo zinastahili kutolewa na watoto.
Sababu zingine ni kuwa wazazi huishi maisha ya afya zaidi kuliko wale wasio na watoto.
0 comments:
Chapisha Maoni