Jumanne, Machi 14, 2017

MARUFUKU YA PUNYETO NA KUMWAGA NJE MBEGU YATINGA MAHAKANI MAREKANI

MWANASIASA mmoja mwanamke, amechukua hatua isiyo ya kawaida katika kile anachosema ni sheria kali za uavyaji mimba kwa kuwalenga wanaume wanaofanya punyeto. Lengo la sheria hiyo yake ni kuwalinda watoto ambao hawajazaliwa kila mahali.
Jessica Farrar ambaye ni mwanachama wa Democratic katika bunge la wawakilishi jimboni hapa, alisema anataka mwanamume atakayemwaga mbegu zake za kiume nje ya uke wa mwanamke ama kutengenezwa nje ya kituo cha matibabu kutozwa faini ya dola 100.
Farrar aliwasilisha bungeni muswada huo nambari 4260, ambao unadai kuwa iwapo mwanamume atapatikana na hatia kwa kumwaga mbegu hizo nje itachukuliwa kama kitendo kibaya dhidi ya mtoto ambaye hajazaliwa.
“Iwapo inaonekana kama hatua isiyo ya kawaida basi hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa” alisema Farrar.
Anajua hautaidhinishwa kuwa sheria lakini anasema kuwa sio rahisi zaidi ya kuwawekea wanawake sheria kali za uavyaji mimba katika jimbo la Texas wakati mtu anapochagua kutaka kuavya mimba.
Hatua yake ya mwisho ilikuwa hivi karibuni kuhusu miswada kadhaa ya wanawake anayosema inapunguza haki za wanawake. Sheria ya hivi karibuni, ilikuwa ile inayowashinikiza wanawake kuchagua kuzika ama kuchoma mabaki ya viinitete kutokana na mimba iliotoka ama ile iliotolewa.
Wakati wa kusikilizwa kwa muswada huo mnamo Agosti mwaka jana, Seneta wa jimbo hilo Don Huffines alisema: kwa muda mrefu sasa Texas imeruhusu viumbe visivyo na hatia kutupwa na uchafu.
Iwapo tunachukulia hatua hizi na umuhimu mkubwa kwa sababu ya maisha, basi, hatuwezi kupoteza hata mbegu moja lakini wakosoaji wake hawakupendelea.
“Huu ni ujinga wa wazi” mtu mmoja alituma ujumbe wake katika mtandao wa Twitter, akisema kuwa “ni yai lililorutubishwa pekee ambalo linahitaji kulindwa akiuliza iwapo angeweza kutumia sheria hiyo dhidi ya wanawake walio katika hedhi.
Jimbo la Texas lina sheria kali za uavyaji mimba nchini, japokuwa mahakama ya juu ilibatilisha marufuku ya uavvaji mimba uliosababishwa na dawa baada ya wiki saba mwaka uliopita.
Sheria hiyo inamaanisha kwamba, kliniki zinazoavya mimba ni chache mno. Kulingana na gazeti la Tribune katika jimbo hilo kulikuwa na kliniki 19 za uavyaji mimba mnamo Juni 2016, nyingi zikifanya kazi katika maeneo ya mijini.

0 comments:

Chapisha Maoni