Jumanne, Machi 14, 2017

RIDHIWANI KIKWETE AHOJIWA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete jana alihojiwa na tume ya kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya. Alipoulizwa kuhusu kuitwa huko, mwenyekiti wa tume hiyo, jaji Siang'a amesema walimuhoji kweli na kila anayetuhumiwa hawatamuacha, watamuita na kumuhoji, wakibaini analo kosa watachukua hatua. 
Amedai yeye anaamini ni bora kukera baadhi ya watu kwa kutenda sahihi ya anachokifahamu kuliko kuridhisha mtu kwa muda ilhali akifahamu akitandacho si sahihi.
Upande wake, Ridhiwani amesema amefurahi kupata fursa ya kueleza ukweli na wamebaini kuwa hauzi wala kusafirisha madawa ya kulevya. 
Amedai roho yake imesuuzika na taharuki iliyokuwepo miongoni mwa jamii kuwa huenda anauza dawa za kulevya sasa ianaondoka.

0 comments:

Chapisha Maoni