Jumatatu, Machi 13, 2017

SERIKALI YA TANZANIA KUKARABATI OLDUVAI GORGE

Serikali ya Tanzania imeanza kukarabati kambi iliyokuwa inatumiwa na watafiti maarufu wa mambo ya kale Dr Luois Leakey na Dr Mary Leakey, iliyopo bonde la Olduvai katika eneo la Ngorongoro.
Waziri wa Maliasili na utalii wa Tanzania Profesa Jumanne Maghembe amesema kambi hiyo inafanyiwa marekebisho ili kurudisha mwonekano kama ilivyokuwa kwenye miaka ya sitini. Watalii na watafiti wataruhusiwa kulala ndani na kujifunza mambo kuhusu binadamu wa kale.

Mwezi Julai mwaka 1959 Dr Leakey aligundua fuvu la binadamu huyo aliyeishi miaka milioni 1.75 iliyopita katika eneo la Ngorongoro.
Msimamizi wa kambi hiyo Bw John Paresso amesema kazi ya kukarabati kambi hiyo itahusisha kurudisha kitanda walichotumia watafiti hao. Na sasa wanawasiliana na familia ya Dr Leakey mjini Nairobi kurudisha kitanda hicho kwenye kambi.

0 comments:

Chapisha Maoni