Jumatatu, Machi 13, 2017

HATARI YA MALI KUONDOLEWA KATIKA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Mali inaweza kuondolewa kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 baada ya Serikali kuwafukuza viongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) halizipi mamlaka Serikali kuingilia mchezo huo na imeshuhudiwa nchi nyingi za Afrika zikifungiwa kwa sababu hiyo.
Licha ya hilo, Waziri wa michezo wa Mali, Mwanasheria Amadou Diarra Yalcouye amesema FIFA haiwezi kuifanya Serikali ibadili uamuzi huo. Muda si mrefu Wizara itaaunda kamati ya muda ya kuendesha na soka.
Mali ilivurunda katika fainali za kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu nchini Gabon.

0 comments:

Chapisha Maoni