Jumatatu, Machi 13, 2017

TAKATAKA ZAUA WATU 35 ADDIS ABABA

Watu zaidi ya 35 wamefariki dunia baada ya lundo kubwa la takataka pembezoni mwa Addis Ababa kuporomoka Jumamosi usiku. Mkurugenzi wa ofisi ya mawasiliano ya serikali ya mji wa Addis Ababa Bw. Dagmawit Moges amesema idadi ya vifo huenda itaongezeka, wakati kazi ya kutafuta watu waliopotea inaendelea kwenye eneo la tukio ambako maporomoko ya takataka yamefunika majengo kadhaa.

0 comments:

Chapisha Maoni